'Diary` yangu (my diary)

Monday, September 5, 2011

Akufaaye kwa dhiki ndiye rafiki wa kweli-23

‘Nilikuwa naomba kuongea na mume wa huyu dada..’ akasema Docta.
‘Unataka kuongea na Mume wake…! Kwanini Docta uongee na mume wake, wakati mimi ndiye nimemleta hapa hospitali?’ akauliza Shangazi wa Maua, na kabla docta hajajibu kitu shangazi akauliza `Kuna matatizo yoyote, maana huyu tulichomleta hapa ni hii habari ya kuchanganyikiwa, na….’ akawa anaongea shangazi akiwa anaonyesha uso wa wasiwasi, akiwaza mbali zaidi kuwa huenda binti yake ana matatizo mazito kinyume anavyomdhania.
‘Huyu mumemlta hapa, na sisi kama kawaida yetu, kwanza tunamchunguza kwa kuchukua vipimo vyote kama tulivyofanya, na….kwa vile bado yupo katika uchunguzi na uchunguzi wa matatizo kama haya sio wa siku moja, inahitaji muda, na baadhi ya vipimo ninavyo, …ndio maana nishauri kuwa ni vyema nikamuona mume wake, kwani kuna mambo mengine yanahitaji kuongea naye kwanza,…’ akasema huyo docta.
‘Mume wake ni marehemu, alifariki miaka miwili iliyopita, na tangu afariki, amekuwa katika hali hii mbaya, haamini, na hasahau, kiasi kwamba imezidi kupita kiasi, ilifikia hatua kama anataka kujiua, mara anatoka usiku na kupotea, na hii hali ndio inatutia mashaka mtu anatoka usiku na anakwenda asipokujua, na anaweza akafanya vitendo usiku, na ikifika asubuhi haui kuwa alifanya nini…’ akaelezea shangazi.
‘Hayo ndio nataka kuyasikia na tatizo kama hili, linahitaji maelezo yote mnayojua kuhusiana na yeye, chanzo chake , nini anakifanya….na pia lazimia tumchunguze afya yake, ikiwezekana kila kipimo, kwasababu mambo mengine yanaweza kutokea, ikazalisha matatizo mengine, …na ndio maana nikashauri hivyo, sasa kama mume wake hayupo, basi ngoja niongee na mgonjwa mwenyewe…’ akasema Docta.
‘Nakuomba tafadhali, kama kuna tatizo ambalo lilihitaji mume wake, ambalo unaona ni muhimu kuwepo mtu wa ziada, naomba uniambie mimi kwanza, kwasababu huyu ni binti yangu na mimi ndiye ninayemjua kuliko mtu yoyote, naomba uniambie mimi mwenyewe…’ akasema Shangazi na kukatisha maneo pale mlango ulipofunguliwa.
Wakati wanaongea na Docta , mlango ulifunguliwa kwa ghafla na akaingia Maua, aliona wamekaa muda mrefu na yeye kaachwa chumba kingine akisubiri, hakuipenda hali na mazingira ya hospitalini, akawa kama anaisikia kichefu chefu, …alitamani atoke akimbie….baadaye akaona awaondeee huko huko ndani awaambie kuwa yeye anaondoka.
‘Docta umeshanichukua vipimo, naomba majibu yake maana kesho nina darasa, siwezi kushinda hapa, nihitaji muda wa maandalizi , naweza kwenda,…au kama majibu ni leo au kuna lolote..?’ akauliza Maua, na Shangazi akamkonyeza docta kumuashiria kuwa asimwambie lolote kwanza.
‘Matatizo yako sio ya kuharakisha, yanahitaji tukae tuongee, kwanza niliona ni vyema tukaanza kwa kuchukua vipimo vyote ili kuhakikisha kuwa hakuna tatizo jingine, na hili ndilo tumelifanya, tunasubiri matokeo yake, na wakati tunasubiri hili nilitaka kujua historia yako , maelezo yako kwa ujumla, …’ akaongea Docta.
‘Kwanini docta yote hayo…? Akauliza Maua na kumwangalia shangazi yake,
‘Maua hapa umeletwa kwa tatizo gani…? Akauliza Docta
‘Hawa ndio wameniambia natakiwa kuja kukuona, lakini mimi Docta sina tatizo lolote, nimeshajijua nini kilikuwa kinanisumbua, ilikuwa ni mawazo mengi, na…’ akawa anaongea Maua huku anatizama saa yake.
‘Sawa kabisa, nakuunga mkono sana, na hivyo ndivyo inatakiwa, lakini kwanini ikafikia hivyo, ukawa na mawazo mengi, kwanini uwe unapoteza fahamu mara kwa mara, hayo na mengine mengi yanatakiwa yachambuliwe na mwisho wake tunakuwa tunapata suluhisho kama mataibabu…ndio tumeshajua kuwa kuna kiini ambacho kimeanzia baada ya kuobdokewa na mume wako…lakini hilo linaweza likawa na sababu ya matatizo uliyokuwa nayo kabla bila kujijua, na sisi kama wataalamu tunatakiwa tunatakiwa tuyagundue hayo…sasa kwanza kabla sijaongea na wewe nilikuwa naomba niongee na mzazi wako, halafu wewe tutaongea na kupangiana siku ya kuonana tena, nakuhakikisha kuwa nitakuwa sichukui muda wako mwingi…’ akasema Docta.
‘Lakini shangazi wewe ndioumenilea, uliwahi kukutana na matatizo kama hayo kutoka kwangu..?’ akamuuliza shangazi yake.
‘Wewe nisubiri kwanza nikaongee na docta, haya tunayotaka kuyafanya ni kwa afya yako, usiwe kama mtoto mdogo wa kulazimishwa kunywa dawa…’ akasema shangazi yake kwa ukali na Maua akanywea  na kutoka mle ndani kwenda kusubiri kile chumba alichokuwa mwanzoni, alipofika hapo akawa anawaza mengi, kwanini huyu docta atake kuongea na shangazi yake wakati yeye ndiye mgonjwa, yeye sio mtoto mdogo…au nina ugonjwa mbaya nini..lakini kweli najisikia siku hizi kuchoka, na…hapana…hapana….siumwi mimi….
 Baadaye shangazi akatoka na kumwambia Maua docta anataka kuongea na yeye, wakaingia kwa docta wakiwa wote wawili, ilionekana shangazi hakutaka kabisa binti yake kuongea na docta wakiwa wawili, akawa yupo pembeni akimsikiliza Docta anavyomuhoji Maua.
‘Maua mengi ya historia yako nimeyasikia toka kwa mzazi wako, lakini hata hivyo wewe siomtoto mdogo, na kwa vile uliwahi kuolewa, tunasema wewe ni mtu mzima, naomba nikuulize swali moja ambalo majibu yake yanaweza kunisaidia katika kazi yangu,…..
                                    **************                        
Maneno alibakia kaduwaa hata kuwakaribisha wageni wake alishindwa, akabakia akiwaangalia kwa mshangao, na wale wageni wakawa wameduwaa pia, hawakuweza kusema kitu wakawa wamesimama pale mlangoni. Na aliyeanza kuongea ni Maua akasema kwa sauti ya kitoto, mtoto anayedeka kwa mzazi wake;
‘Untie, mimi napoteza muda wangu ,hapa sasa hivi nina miadi na watu wangu, naomba niondoke, mimi sina mazungumzo na…huyo mtu wako, akanyosha kidole kimuonyeshea Maneno, na kitendo kile kilimfanya Maneno ashangae na hapo akazindukana kutoka kwenye ule mshangao na kuanza kuwakaribisha, na wakati anafnya hili macho yake yalikuwa kwa Maua, alishangaa kumuona alivyobadilika, kwa kipindi cha miezi kadhaa ambacho hakuwa wanaonana kumetokea mabadiliko makubwa, Maua kanenepa kawa mweupe zaidi ya weupe wake…
‘Sawa Maua kama hiyo kazi yako ni muhimu sana, wewe nenda , lakini tafuta muda muafaka tuongee kwa marefu na mapana, na kama una tatizo hakikisha unaniambia, sasa hivi nataka tuwe karibu kuliko muda wowote ule, kwani nimeongea na docta wako kwa kirefu,…usiione kuwa u mzima,…’ akasema shangazi, huki akimkagua Maua maumbile yake.
‘Shangazi , mimi sina matatizo kwa sasa, nimeshapona, na nakuhakikishia kuwa kazi yangu hii ndiyo tiba yangu, sitakimatibabu mengine…’ akasema halafu kama vile kakumbuka , akamgeukia Maneno na kumsalimia na kumuomba samahani kuwa hakumsalimia kabla. Maneno akamjibu kuwa hakuna mataizo ila hata yeye anaomba msamaha kwa kutowakribisha na kubakia kuwashangaa, aliwashangaa kwa kuwa wameongozana..halafu akamalizia kwa kuulizia hali yake Maua kwa sababu amesikia kuwa wametoka kwa docta,
‘Mimi sijambo, ila shngazi kama ulivyo wewe alitaka nikamuone huyo docta bingwa wenu, amaenihoji maswali mengi utafikiri mimi ni mfungwa, mwisho wa siku akaniambia natakiwa mara kwa mara niwe namtembelea, lakini….’ Akabenua mdomo na kutaka kuondoka, akaanga kwa kusema kuwa sasa hivi hana nafasi ya kukutana kutana na watu kutokana na ratiba yake,..
‘Lakini hata hivyo mbona simu yako nakupigia haipatikani, umebadili namba …?’ akauliza Maneno.
‘Mara nyingi natumia namba zao walizonipa, kwasababau ya kuogopa usumbufu, wakati upo darasanai watu wanakupigia, haileti picha mbaya, namba ile bado ipo, ila kwa muda nikiwa sina kazi..’ akasema Maua na kuondoka zake….
Walibakia shangazi na Maneno wakiongea, na ilionekana walichokuwa wakiongea ni jambo zito sana, jambo ambaloo lilimafanya Maneno achanagnyikiwe, , lakini mwisho wa siku walifikia muafaka kuwa Maneno ahakikishe ameonana na Maua …
                                                        ***********
‘Halloh, mimi ni Maneno , Maua, nakuomba tuonane , nina jambo kubwa, na muhimu nataka kuongea na wewe, na naomba ikiwezekana kama ratiba yako haina nafasi uombe zarura, hili jambo ni muhimu sana…’ akasema Maneno.
‘Sawa, fika nyumbani nip oleo nyumbeni , tuna mapumziko ya siku nzima leo, ..’ akasema Maua.
Maneno liondoka kwake hadi nyumbani kwa Maua, alipofika alimkuta kakaa kwenye kochi, na alipomuangalia alimuona kama ana mawazo mwengi sana, hakutaka kudadisi zaidi akaanza kuongea mambo mengine kama kuvuta muda kabla hajafikia lengo lake, na hapo Maua akaona anapotezewa muda akauliza.
‘Nakumbuka kwenye simu umeniambia kuwa una jambo muhimu unataka kuniambia, naomba uniambie, sipendi kuwekwa rehani,,!’ akasema Maua
‘ Maua, kuna usemi usemao kuwa kila jambo hutokea ili iwe sababu, na huenda inatokea hivyo ili iwe heri kwa wanadamu. Naomba unielewe Maua kuwa sina maana mbaya, na sikutakii mabaya katika masiha yako. Nakurejesha kidogo nyuma, siku ile tulipokuwa Arusha, nakumbuka uliniuliza maswali mengi na mojawapo ya mswali yako nilishindwa kukujibu, leo nimekuja nikiwa tayari na majibu yake, kwani nilihitaji muda wa kutafakari sana kabla sijakujibu.
‘Maswaligani shemeji, mimi nakuomba tusikumbushane yaliyopita na hata docta alinishauri hivyo, kama ni hayo yamepita na nimeshasahau, …kwani yana msingi gani kwako hayo maswali?’ akauliza Maua.
‘Yana msingi mkubwa sana, yana maana kubwa sana kwangu na kwako, unakumbuka uliniuliza ni nani aliyekuokoa siku ile, ambaye ndiye alikubeba hadi chumbani kwako,,? Akauliza Maneno bila kujali maneno ya Maua kuwa hataki kukumbushwa yaliyopita.
‘Ilikuwa ni ndoto, najua wewe ulitaka kunichezea akaili yangu, ningeliwezeje kutoka usiku hadi kwenye pori la hatari, na sizani kuwa kuna joka kubwa kama lile..ilikuwa ni ndoto na wala sitaki kujikumbusha kichwni.
‘Mua ilikuwa sio ndoto, ni kweli tupo yaliyotokea siku ile….’ Akasema Maneno na kumwangalia machoni Maua, na Maua alikuwa kama anatafakari kitu, halafu akauliza kaam ilikuwa ni ndoto, ni nani basi aliniokoa ni nani aliyenibebea hadi chumbani kwangu , na ni nani aliyelela name siku ile….’ Akauliza Maua akiwa bado anatafakari kwa undani, alionekana kuwa na mawazo mazito, na kumfanya Maneno awe na mashaka kwa hayo anayotaka kumwambia, aliombea ingeliwezekana shangazi yake angelikuwepo, lakini kutoka a makubaliaono yao, huo ni mzigo wake, vinginevyo aatkwenda kuozea jela….
‘Maua, ile haikuwa doto, mimi ndiye niliyekuokeoa kutoka kwenye lile joka,nikakubeba hadi chumbani kwako…’ akasema Maneno. Na hapo hapo Maua akainuka palealipokuwa kakaa na kumwangalai Maneno kwa hasira, …na machozi yakaanza kumtoka kama mvua, …na baadaye akaanza kulia kwa kwikwi…
Baadaye akanyamaza na kumwangalia Maneno na kusema `wewe nishetani, wewe ni muangamizi mkubwa, ina maana wewe ndiye tuliyelala naye usiku na sio Mhuja sio, wewe ndio ulichukua matatizo yangu ili uinufaishe nafasi na tamaa yako sio…unajifanya mpole, unajifanya una huruma, kumbe nia na lango lako lote lilikuwa hivyo, una maana gani, unajifanya ulikuwa rafiki mwema wa Mhuja, kumbe lengo lako ni ingine kabisa….ulinifanya nini usiku ule, nakuombe uniweke wazi, ….? Akauliza Maua.
‘Maua nakuapia kwa mungu kuwa mimi sikumbuki kukulazimisha…mimi nilishitukia tu tupo kwenye tendo hilo, na …ooh, shemeji nisamahe sana, sikuwa na nia hiyo mbaya, ….nakuomba sana nipo chini ya miguu yako..’ akasema Maneno hadi kupiga magoti, lakini alikuwa bado yupo mbali na aliposimama Maua akainua kichwa kuangali juu, alikuwa kama anamuomba Mungu wake, alikuwa anaomba kitu kikubwa kuwa kimpishie mmbali na Maneno alikuwa na hamu ya kujua nini anachokiomba…
 Maneno akamwangalia Maua machoni, lakini hata pale Maua alipotizama chini hakuweza kumtizama Maneno machoni. Maua alikuwa sasa kaangali chini, alikuwa hana nguvu ya kumtizama shemji yake machoni, alikuwa haamini maneno aliyoyasikia sasa hivi kutoka kwa shemeji yake kuwa ndivyo ilivyotokea usiku ule, alishafikia tamati kuwa ile ilikuwa ni ndoto, na hata kuanza kusahau, sasa habari hii inamtonesha, na inamti amaozi makubwa sana…na hapo akaumbuka siku ile ilivyokuwa;
 Siku ile alipoamuka asubuhi  alijipa moyo kuwa ile ilikuwa ni ndoto, lakini kadri muda ulivyokwenda na kutafakari vyema aliiona kuwa ni kweli na kuwa lile tendo lilifanyika kiukweli, alikumbuka jinsi alivyokuwa akimtizama shemeji yake siku ile, lakini sheemji yake alikuwa hamtizami machoni,…na kuna muda aliwaza hivyo kuwa huneda, labda ndiye alifanya ujanja wote huo, ili amfanyie hayo ambayo leo anadhihirishiwa kuwa ndivyo, hapo chuki ikaanza kumjaa Maua moyoni mwake, alitamani kama kungelikuwa na silaha ….
‘Lakini kwanini nimekuwa mjinga wa kujidanganya, ni lazima nikubali ukweli kuwa mume wangu keshakufa na lolote linalotokea leo kuhusu yeye, kumuota na…hayo yote ni mawazo tu..’ akawaza na kutafakari hivyo, akamwangalia Maneno, ambaye likuwa anamtizama kwa uwoga na halafu akageuka na kutizama pembeni na bila kujijua akasema kwa sauti  ‘Lakini mume wangu ni marehemu …’
‘Huo ndio ukweli ulivyo Maua ukubali kwenye nafsi yako kuwa Mhuja hayupo hapa duniani tena ni marehemu’ akasema Maneno aliposikia kauli hiyo, na kupata nguvu kuwa sasa anaweza kuongea kile alichotaka kusema. Na Maua aliposikia kauli hiyo ya Maneno akili yake ikawa kama imezibuliwa na kuwa kwenye dunia nyingine tena, ikatoka kule kwenye mawazo ya kwanza na kwenda mbali zaidi ya kuwaza akawa sasa anamuona mtu, ingawaje anayemtizama kwa wakati ule ni Maneno, lakini alikuwa hamuoni Maneno, kwa mbele yake alikuwa akimtizama mtu mwingine tofauti, alikuwa akimtizama Mhuja…na sura yake ilipojaa mbele yake, machozi yakaanza kumtoka kwa fujo….
Maneno alipoona kuwa Maua anamtizama yeye huku analia, akajua sasa anasikilizwa na kulia kule huenda kukasaidia kuondoa yale yote yanayomzonga moyoni, akaendelea kuongea kwa kusema ‘Maua hebu jiulize wewe mwenyewe, familia ya akina Mhuja mwaka huu wamesoma dua ya kuwaombea waliotangulia kama unavyokumbuka na katika orodha ya marehemu jina lake lilikuwa la kwanza kutajwa kwa kurehemewa, …hebu jiulize kama wangekuwa na mawazo kama yako wangelifanya hivyo, ina maana wao kweli hawana uchungu na mtoto wao…?’ akauliza Maneno na kumwangalia Maua ambaye alikuwa bado anabubujikwa machozi kama mvua.
 Maneno akamtizama Maua kusubiri kuwa atasema lolote, alichoona ni mtu kamkodolea macho huku akiwa anatokwa na machozi, akasita kidgo kuongea lakini baadaye akasema `Maua leo niomekuja kwako maalumu kukuambia jambo muhimu sana, ….naomba unielewe, kuwa silisemi himi kwasababu ya shinikizo la matatizo yako, nalifanya kwa kuwa nina nia  nalo….’ Akasita kuongea na kumtizama Maua, cha ajabu alimuona akiwa bado kamkodolea macho, nay eye akatizama pembeni na kusema.
Maua hata kama unajiona kuwa umepona, lakini kwangu mimi, hata kwa shangazi yako na hata docta tumeliona hili kuwa bado hujapona, na docta kashauri kuwa bado una matatizo , matatizo ambayo yanahitaji mtu wa kuwa karibu naye wakati wote…lazimia uwe na mtu anayekufahamu fika, kwa mfano anaweza akaa rafiki yako akakuuliza mambo yaliyopita, akakurudishia uchungu, kaondoka wewe huku nyuma, ukaanza kubadilika na labda ni usiku, ukatoka na kwenda kusikojulikana…nakutolea huu mfano kwasababu huishi peke yako katika  hii dunia, watu kama hawo wasiokujua watatokea na kukuumiza moyo wako, licha ya kuwa nia yako ni kusahau kabisa, lakini ukikumbushwa hayo utakuwa unarejeshwa kwenye majonzi, na inawezekana kabisa yakatokea kama yale ya Arusha, na je kwa muda huo utakuwa na nani anayekujua vyema….. ‘ Maneno  akawa anaongea na kurudia rudia maneno kwa msisitizo, na akawa sasa kama anamsogelea, akijaribu kuona Maua atafanya nini akimsogelea karibu, lakini alichoona ni mtu kumtizama tu huku analia
Baadaye Maua akatulia na kupikicha macho yake, akawa kama vile kazindukana toka katika dimbwi lile la mawazo, akahema kwa nguvu, halafu akatizam tena kwa mbele, sasa akawa hamuoni yule aliyekuwa akimtizama mwanzoni, yupo Maneno , yupi sheei yake, ambaye analeta habari asizozitaka…..Maua alimtizama Maneno kwa mcho ya chuki, akawa kama anataka kumwambia usinisogelee, shetani mkubwa wee, lakini hayo yalikuwa akilini mwake, akawa anamwangalia tu kwa macho hayo ya chuki, yakiwa yamegubikwa na wingu la machozi…
‘Maua kwa ujumla kwa usalama wako unahitaji mtu wa kukaa nawe karibu, si usiku wala mchana, hebu nikuulize kweli ilikuwaje hadi ukatoka usiku kama ule hadi maporini sehemu ambayo usingeweza kwenda mwenyewe ukiwa na akili zako kamili, huoni kuwa umekumbwa na ule ugonjwa…ugonjwa unaomfanya mtu afanye matendo akiwa usingizini…, wewe ninavyokujua unaogopa sana nyoka hata kuitizama kwenye runinga hutaki, lakini siku ile ulikuwa nalo mwilini mwako, limekuzingira…hebu fikiria…kwa ujumla unahitaji mtu wa kuwa naye karibu, la sivyo tutasikia mengine, na mimi sitakubali hilo…’ akasema Maneno na moyoni Maua akasema ndio maana ukafanya ushetani wako huo, lakini hakutoa kauli hiyo kwa nguvu, hakutamani kuongea kwani kama angeliongea angesema maneno machafu na mwisho angekumbwa na balaa jingine, akabakia kimiya na hata kufunga macho yake.
‘Maua samahani najaribu kukurudisha nyuma, ili uone hatari iliyopo mbele yako…hebu jiulize wewe mwenyewe siku ile ulitokaje ndani na kutokomea maporini, na huku ushindwe kutoka na kutokomea mjini au hata baharini, na kwa ujumla hali kama hiyo unaweza ukawa uantembea bila kujali mgari au nini, kwasababu wazo lako linakuwa kufanya jambo moja, na mengine huyaoni…’ akasema Maneno…na hapo Maua akayafungua macho yake na kitu kama uwoga ukamwingia, kuonyesha naye anaikumbuka ile siku, ….analiona lile joka aliloliona kwenye njozi…ooh, sio njozi eti ilikuwa ni kweli…akazidi kufunua macho kwa woga, kama vile analihisi lile joka lipo karibu yake…
‘Sasa Maua nakuomba sana, sio kwamba nachukulia nafasi hii kama kisingizio, lakini …nafanya hili nikiwa nahitaji, nikiwa natamani, nikuwa na upendo wa dhati kwako. Mimi na Mhuja tulikuwa marafiki, tulikuwa tukipendana zaidi ya ndugu na wakati mwingine tulikuwa tukitaniana kuwa `mke wake ni wangu na mke wangu ni wake’ ulikuwa ni utani, lakini sasa naona imefikia mahali kukiri kuwa natamani iwe hivyo…naomba iwe hivyo…Maua nakuomba kwa mikono miwili nakuomba unipe nafasi ya Mhuja…’ akatulia na kumwangalia Maua
Maneno alimshngaa Maua kuwa haonyeshi dalili yoyote ya kukubali au kukataa, na inaoenakan kama vile hayupo hapo kabisa, alikuwa katulia kimiya kama vile hajamsikia na Maneno akaendelea kuongea kwa kusema, `Mhuja kaondoka,na kiukweli kunahitajika mtu kuziba nafasi yake…na mtu huyo ni mtu anayekujali, anayekufahamu na anayekupenda kwa moyo wake wote, kama alivyokuwepo Mhua nap engine akakupenda zaidi yake, huwezi jua, …na Maua mtu huyo, hayupo mbali nawe, mimi ninakuahidi kuwa hutajijutia…nakuomba tafadhali unikubalie ombi langu la mimi kuichukua nafasi ya rafiki yangu mpendwa, …’ akasema Maneno a kushika kifuani kwake kwa mikono miwili.
‘Maua kiukweli mtu huyo anahitajika kwako haraka iwezekanavyo, na mimi ndiye ninayefaa, kwa sifa zote nilizozitaja, …hata hivyo baada ya tukio lile la Arusha, nimekuwa nikiteseka sana, kwasababu tendo lile lilitokea bila dhamira yangu…sikujiela ilikuwaje …na siwezi kuvumilia zidi na hata hivyo nitashindwa  kabisa kukuangalia machoni, najisikia uchungu sana, nasononeka sana….Nakuomba unisamehe kwasababu lile limetokea na huenda limetokea ili iwe hivyo..…’ akasema Maneno huku akimsogelea Maua na kuja kumpigia magoti...’
Maua alibakia akiwa kama kashikwa na mshangao, halafu akawa anawaza kwa undani nini alichoambiwa, na mara ile taswira ya Mhuja ikatokea tena mbele yake. Sasa hivi ila taswira ilikuwa kama anamwangalia kwa macho ya kutaka kujua atatoa kauli gani, na uso wa hiyo taswira ulionyesha chuki, ukiwa kama unasema `wewe ni msaliti, wewe umefanya nini, …’ Maua kuhis hivyo akageuza kichwa kutizama pembeni lakini akakutana na taswira ile ile, sasa ikimwambia `unaona ulivyo mnafiki, hata kuniangalia unaishindwa, kwasababu umenisaliti…wewe ni msaliti..’ akageuka huku na tena akakutana na uso kama ule ukimwambia; `haya toa jibu..toa jibu, …na jibu gani utaweza kulitoa wakati umeshafanya kwa vitendo, ..iliyobaki ni kauli kwa watu lakini kwa mtendo umeshatoa jibu…mkubalie msaliti mwenzako…kwaheri, nakutakia mafanikio mema…’ Maua liposikia maneno hayo kihisia akaanza kulia na kusema kwa sauti.
‘Hapana mimi sio msaliti  Mhuja, katu sikutarajia kufanya hivyo… na wala sikujua kuwa imekuwa hivyo…nilijua ni ndoto…hapana siwezi kukusaliti Mhuja, ….nakupenda mume wangu, nakuomba usiniache…nakuomba tafadhali,…sijui kilitokea kitu gani mpaka ikatokea hivyo…..sijui, na sijui na kitu gani kinanilazimisha kufanya hivyo….nakuomba Mhuja unisamehe, nipo tayari kuja huko ulipo, nipo tayari..hata sasa, nipo tayari…oooh, mungu wangu nimefanya nini…nisamehe mungu wangu….mungu wangu nakuomba unichukue roho yangu ikaonane na mume wangu…ooooh’ Akashikwa na kitu kama kizungu zungu akadondoka chini  na kupoteza fahamu...

‘Nilikuwa naomba kuongea na mume wa huyu dada..’ akasema Docta.
‘Unataka kuongea na Mume wake…! Kwanini Docta uongee na mume wake, wakati mimi ndiye nimemleta hapa hospitali?’ akauliza Shangazi wa Maua, na kabla docta hajajibu kitu shangazi akauliza `Kuna matatizo yoyote, maana huyu tulichomleta hapa ni hii habari ya kuchanganyikiwa, na….’ akawa anaongea shangazi akiwa anaonyesha uso wa wasiwasi, akiwaza mbali zaidi kuwa huenda binti yake ana matatizo mazito kinyume anavyomdhania.

‘Huyu mumemlta hapa, na sisi kama kawaida yetu, kwanza tunamchunguza kwa kuchukua vipimo vyote kama tulivyofanya, na….kwa vile bado yupo katika uchunguzi na uchunguzi wa matatizo kama haya sio wa siku moja, inahitaji muda, na baadhi ya vipimo ninavyo, …ndio maana nishauri kuwa ni vyema nikamuona mume wake, kwani kuna mambo mengine yanahitaji kuongea naye kwanza,…’ akasema huyo docta.

‘Mume wake ni marehemu, alifariki miaka miwili iliyopita, na tangu afariki, amekuwa katika hali hii mbaya, haamini, na hasahau, kiasi kwamba imezidi kupita kiasi, ilifikia hatua kama anataka kujiua, mara anatoka usiku na kupotea, na hii hali ndio inatutia mashaka mtu anatoka usiku na anakwenda asipokujua, na anaweza akafanya vitendo usiku, na ikifika asubuhi haui kuwa alifanya nini…’ akaelezea shangazi.

‘Hayo ndio nataka kuyasikia na tatizo kama hili, linahitaji maelezo yote mnayojua kuhusiana na yeye, chanzo chake , nini anakifanya….na pia lazimia tumchunguze afya yake, ikiwezekana kila kipimo, kwasababu mambo mengine yanaweza kutokea, ikazalisha matatizo mengine, …na ndio maana nikashauri hivyo, sasa kama mume wake hayupo, basi ngoja niongee na mgonjwa mwenyewe…’ akasema Docta.

‘Nakuomba tafadhali, kama kuna tatizo ambalo lilihitaji mume wake, ambalo unaona ni muhimu kuwepo mtu wa ziada, naomba uniambie mimi kwanza, kwasababu huyu ni binti yangu na mimi ndiye ninayemjua kuliko mtu yoyote, naomba uniambie mimi mwenyewe…’ akasema Shangazi na kukatisha maneno pale mlango ulipofunguliwa....

Mlango ulipofunguliwa wote wakakaa kimiya kwani aliyeingia ni Maua, kwani Maua alipoona wamekaa muda mrefu na yeye kaachwa chumba kingine akisubiri akashindwa kuvumilia. Na hata ile hali ya hospitali, harufu ya madawa, akawa kama anaisikia kichefu chefu, …alitamani atoke akimbie….baadaye akaona awaondeee huko huko ndani awaambie kuwa yeye anaondoka.

‘Docta umeshanichukua vipimo, naomba majibu yake maana kesho nina darasa, siwezi kushinda hapa, nihitaji muda wa maandalizi , naweza kwenda,…au kama majibu ni leo au kuna lolote..?’ akauliza Maua, na Shangazi akamkonyeza docta kumuashiria kuwa asimwambie lolote kwanza.

‘Matatizo yako sio ya kuharakisha, yanahitaji tukae tuongee, kwanza niliona ni vyema tukaanza kwa kuchukua vipimo vyote ili kuhakikisha kuwa hakuna tatizo jingine, na hili ndilo tumelifanya, tunasubiri matokeo yake, na wakati tunasubiri hili nilitaka kujua historia yako , maelezo yako kwa ujumla, …’ akaongea Docta.

‘Kwanini docta yote hayo…? Akauliza Maua na kumwangalia shangazi yake,

‘Maua hapa umeletwa kwa tatizo gani…? Akauliza Docta

‘Hawa ndio wameniambia natakiwa kuja kukuona, lakini mimi Docta sina tatizo lolote, nimeshajijua nini kilikuwa kinanisumbua, ilikuwa ni mawazo mengi, na…’ akawa anaongea Maua huku anatizama saa yake.

‘Sawa kabisa, nakuunga mkono sana, na hivyo ndivyo inatakiwa, lakini kwanini ikafikia hivyo, ukawa na mawazo mengi, kwanini uwe unapoteza fahamu mara kwa mara, hayo na mengine mengi yanatakiwa yachambuliwe na mwisho wake tunakuwa tunapata suluhisho kama mataibabu…ndio tumeshajua kuwa kuna kiini ambacho kimeanzia baada ya kuobdokewa na mume wako…lakini hilo linaweza likawa na sababu ya matatizo uliyokuwa nayo kabla bila kujijua, na sisi kama wataalamu tunatakiwa tunatakiwa tuyagundue hayo…sasa kwanza kabla sijaongea na wewe nilikuwa naomba niongee na mzazi wako, halafu wewe tutaongea na kupangiana siku ya kuonana tena, nakuhakikisha kuwa nitakuwa sichukui muda wako mwingi…’ akasema Docta.

‘Lakini shangazi wewe ndioumenilea, uliwahi kukutana na matatizo kama hayo kutoka kwangu..?’ akamuuliza shangazi yake.

‘Wewe nisubiri kwanza nikaongee na docta, haya tunayotaka kuyafanya ni kwa afya yako, usiwe kama mtoto mdogo wa kulazimishwa kunywa dawa…’ akasema shangazi yake kwa ukali na Maua akanywea  na kutoka mle ndani kwenda kusubiri kile chumba alichokuwa mwanzoni, alipofika hapo akawa anawaza mengi, kwanini huyu docta atake kuongea na shangazi yake wakati yeye ndiye mgonjwa, yeye sio mtoto mdogo…au nina ugonjwa mbaya nini..lakini kweli najisikia siku hizi kuchoka, na…hapana…hapana….siumwi mimi….

 Baadaye shangazi akatoka na kumwambia Maua docta anataka kuongea na yeye, wakaingia kwa docta wakiwa wote wawili, ilionekana shangazi hakutaka kabisa binti yake kuongea na docta wakiwa wawili, akawa yupo pembeni akimsikiliza Docta anavyomuhoji Maua.

‘Maua mengi ya historia yako nimeyasikia toka kwa mzazi wako, lakini hata hivyo wewe siomtoto mdogo, na kwa vile uliwahi kuolewa, tunasema wewe ni mtu mzima, naomba nikuulize swali moja ambalo majibu yake yanaweza kunisaidia katika kazi yangu,…..

                                    **************                        
Maneno alibakia kaduwaa hata kuwakaribisha wageni wake alishindwa, akabakia akiwaangalia kwa mshangao, na wale wageni wakawa wameduwaa pia, hawakuweza kusema kitu wakawa wamesimama pale mlangoni. Na aliyeanza kuongea ni Maua akasema kwa sauti ya kitoto, mtoto anayedeka kwa mzazi wake;

‘Untie, mimi napoteza muda wangu ,hapa sasa hivi nina miadi na watu wangu, naomba niondoke, mimi sina mazungumzo na…huyo mtu wako, akanyosha kidole kimuonyeshea Maneno, na kitendo kile kilimfanya Maneno ashangae na hapo akazindukana kutoka kwenye ule mshangao na kuanza kuwakaribisha, na wakati anafnya hili macho yake yalikuwa kwa Maua, alishangaa kumuona alivyobadilika, kwa kipindi cha miezi kadhaa ambacho hakuwa wanaonana kumetokea mabadiliko makubwa, Maua kanenepa kawa mweupe zaidi ya weupe wake…

‘Sawa Maua kama hiyo kazi yako ni muhimu sana, wewe nenda , lakini tafuta muda muafaka tuongee kwa marefu na mapana, na kama una tatizo hakikisha unaniambia, sasa hivi nataka tuwe karibu kuliko muda wowote ule, kwani nimeongea na docta wako kwa kirefu,…usiione kuwa u mzima,…’ akasema shangazi, huki akimkagua Maua maumbile yake.

‘Shangazi , mimi sina matatizo kwa sasa, nimeshapona, na nakuhakikishia kuwa kazi yangu hii ndiyo tiba yangu, sitakimatibabu mengine…’ akasema halafu kama vile kakumbuka , akamgeukia Maneno na kumsalimia na kumuomba samahani kuwa hakumsalimia kabla. Maneno akamjibu kuwa hakuna mataizo ila hata yeye anaomba msamaha kwa kutowakribisha na kubakia kuwashangaa, aliwashangaa kwa kuwa wameongozana..halafu akamalizia kwa kuulizia hali yake Maua kwa sababu amesikia kuwa wametoka kwa docta,

‘Mimi sijambo, ila shngazi kama ulivyo wewe alitaka nikamuone huyo docta bingwa wenu, amaenihoji maswali mengi utafikiri mimi ni mfungwa, mwisho wa siku akaniambia natakiwa mara kwa mara niwe namtembelea, lakini….’ Akabenua mdomo na kutaka kuondoka, akaanga kwa kusema kuwa sasa hivi hana nafasi ya kukutana kutana na watu kutokana na ratiba yake,..

‘Lakini hata hivyo mbona simu yako nakupigia haipatikani, umebadili namba …?’ akauliza Maneno.
‘Mara nyingi natumia namba zao walizonipa, kwasababau ya kuogopa usumbufu, wakati upo darasanai watu wanakupigia, haileti picha mbaya, namba ile bado ipo, ila kwa muda nikiwa sina kazi..’ akasema Maua na kuondoka zake….

Walibakia shangazi na Maneno wakiongea, na ilionekana walichokuwa wakiongea ni jambo zito sana, jambo ambaloo lilimafanya Maneno achanagnyikiwe, , lakini mwisho wa siku walifikia muafaka kuwa Maneno ahakikishe ameonana na Maua …

                                                        ***********
‘Halloh, mimi ni Maneno , Maua, nakuomba tuonane , nina jambo kubwa, na muhimu nataka kuongea na wewe, na naomba ikiwezekana kama ratiba yako haina nafasi uombe zarura, hili jambo ni muhimu sana…’ akasema Maneno.

‘Sawa, fika nyumbani nip oleo nyumbeni , tuna mapumziko ya siku nzima leo, ..’ akasema Maua.
Maneno liondoka kwake hadi nyumbani kwa Maua, alipofika alimkuta kakaa kwenye kochi, na alipomuangalia alimuona kama ana mawazo mwengi sana, hakutaka kudadisi zaidi akaanza kuongea mambo mengine kama kuvuta muda kabla hajafikia lengo lake, na hapo Maua akaona anapotezewa muda akauliza.
‘Nakumbuka kwenye simu umeniambia kuwa una jambo muhimu unataka kuniambia, naomba uniambie, sipendi kuwekwa rehani,,!’ akasema Maua

‘ Maua, kuna usemi usemao kuwa kila jambo hutokea ili iwe sababu, na huenda inatokea hivyo ili iwe heri kwa wanadamu. Naomba unielewe Maua kuwa sina maana mbaya, na sikutakii mabaya katika masiha yako. Nakurejesha kidogo nyuma, siku ile tulipokuwa Arusha, nakumbuka uliniuliza maswali mengi na mojawapo ya mswali yako nilishindwa kukujibu, leo nimekuja nikiwa tayari na majibu yake, kwani nilihitaji muda wa kutafakari sana kabla sijakujibu.

‘Maswaligani shemeji, mimi nakuomba tusikumbushane yaliyopita na hata docta alinishauri hivyo, kama ni hayo yamepita na nimeshasahau, …kwani yana msingi gani kwako hayo maswali?’ akauliza Maua.
‘Yana msingi mkubwa sana, yana maana kubwa sana kwangu na kwako, unakumbuka uliniuliza ni nani aliyekuokoa siku ile, ambaye ndiye alikubeba hadi chumbani kwako,,? Akauliza Maneno bila kujali maneno ya Maua kuwa hataki kukumbushwa yaliyopita.

‘Ilikuwa ni ndoto, najua wewe ulitaka kunichezea akaili yangu, ningeliwezeje kutoka usiku hadi kwenye pori la hatari, na sizani kuwa kuna joka kubwa kama lile..ilikuwa ni ndoto na wala sitaki kujikumbusha kichwni...

‘Maua ilikuwa sio ndoto, ni kweli tupo yaliyotokea siku ile….’ Akasema Maneno na kumwangalia machoni Maua, na Maua alikuwa kama anatafakari kitu...,!
Halafu akauliza 'Kama ilikuwa ni ndoto, ni nani basi aliniokoa ambaye najua ndiye aliyenibaba hadi chumbani kwangu , na najua ndio huyo huyo tulialala naye siku ile….’ Akauliza Maua akiwa bado anatafakari kwa undani, alionekana kuwa na mawazo mazito, na kumfanya Maneno awe na mashaka kwa hayo anayotaka kumwambia, aliombea ingeliwezekana shangazi yake angelikuwepo hapo akamsaidia kuliweka sawa, lakini kutoka na makubaliaono yao, huo ni mzigo wake, vinginevyo atakwenda kuozea jela….

‘Maua, ile haikuwa doto, mimi ndiye niliyekuokeoa kutoka kwenye lile joka,nikakubeba hadi chumbani kwako…’ akasema Maneno. Na hapo hapo Maua akainuka palealipokuwa kakaa na kumwangalai Maneno kwa hasira, …na machozi yakaanza kumtoka kama mvua, …na baadaye akaanza kulia kwa kwikwi…

Baadaye akanyamaza na kumwangalia Maneno na kusema `wewe nishetani, wewe ni muangamizi mkubwa, ina maana wewe ndiye tuliyelala naye usiku na sio Mhuja sio, wewe ndio ulichukua matatizo yangu ili uinufaishe nafasi na tamaa yako sio…unajifanya mpole, unajifanya una huruma, kumbe nia na lango lako lote lilikuwa hivyo, una maana gani, unajifanya ulikuwa rafiki mwema wa Mhuja, kumbe lengo lako ni ingine kabisa….ulinifanya nini usiku ule, nakuombe uniweke wazi, ….? Akauliza Maua.

‘Maua nakuapia kwa mungu kuwa mimi sikumbuki kukulazimisha…mimi nilishitukia tu tupo kwenye tendo hilo, na …ooh, shemeji nisamahe sana, sikuwa na nia hiyo mbaya, ….nakuomba sana nipo chini ya miguu yako..’ akasema Maneno hadi kupiga magoti, lakini alikuwa bado yupo mbali na aliposimama Maua akainua kichwa kuangali juu, alikuwa kama anamuomba Mungu wake, alikuwa anaomba kitu kikubwa kuwa kimpishie mmbali na Maneno alikuwa na hamu ya kujua nini anachokiomba…

 Maneno akamwangalia Maua machoni, lakini hata pale Maua alipotizama chini hakuweza kumtizama Maneno machoni. Maua alikuwa sasa kaangali chini, alikuwa hana nguvu ya kumtizama shemji yake machoni, alikuwa haamini maneno aliyoyasikia sasa hivi kutoka kwa shemeji yake kuwa ndivyo ilivyotokea usiku ule, alishafikia tamati kuwa ile ilikuwa ni ndoto, na hata kuanza kusahau, sasa habari hii inamtonesha, na inamti amaozi makubwa sana…na hapo akaumbuka siku ile ilivyokuwa;

 Siku ile alipoamuka asubuhi  alijipa moyo kuwa ile ilikuwa ni ndoto, lakini kadri muda ulivyokwenda na kutafakari vyema aliiona kuwa ni kweli na kuwa lile tendo lilifanyika kiukweli, alikumbuka jinsi alivyokuwa akimtizama shemeji yake siku ile, lakini sheemji yake alikuwa hamtizami machoni,…na kuna muda aliwaza hivyo kuwa huneda, labda ndiye alifanya ujanja wote huo, ili amfanyie hayo ambayo leo anadhihirishiwa kuwa ndivyo, hapo chuki ikaanza kumjaa Maua moyoni mwake, alitamani kama kungelikuwa na silaha ….

‘Lakini kwanini nimekuwa mjinga wa kujidanganya, ni lazima nikubali ukweli kuwa mume wangu keshakufa na lolote linalotokea leo kuhusu yeye, kumuota na…hayo yote ni mawazo tu..’ akawaza na kutafakari hivyo, akamwangalia Maneno, ambaye likuwa anamtizama kwa uwoga na halafu akageuka na kutizama pembeni na bila kujijua akasema kwa sauti  ‘Lakini mume wangu ni marehemu …’

‘Huo ndio ukweli ulivyo Maua ukubali kwenye nafsi yako kuwa Mhuja hayupo hapa duniani tena ni marehemu’ akasema Maneno aliposikia kauli hiyo, na kupata nguvu kuwa sasa anaweza kuongea kile alichotaka kusema. Na Maua aliposikia kauli hiyo ya Maneno akili yake ikawa kama imezibuliwa na kuwa kwenye dunia nyingine tena, ikatoka kule kwenye mawazo ya kwanza na kwenda mbali zaidi ya kuwaza akawa sasa anamuona mtu, ingawaje anayemtizama kwa wakati ule ni Maneno, lakini alikuwa hamuoni Maneno, kwa mbele yake alikuwa akimtizama mtu mwingine tofauti, alikuwa akimtizama Mhuja…na sura yake ilipojaa mbele yake, machozi yakaanza kumtoka kwa fujo….

Maneno alipoona kuwa Maua anamtizama yeye huku analia, akajua sasa anasikilizwa na kulia kule huenda kukasaidia kuondoa yale yote yanayomzonga moyoni, akaendelea kuongea kwa kusema ‘Maua hebu jiulize wewe mwenyewe, familia ya akina Mhuja mwaka huu wamesoma dua ya kuwaombea waliotangulia kama unavyokumbuka na katika orodha ya marehemu jina lake lilikuwa la kwanza kutajwa kwa kurehemewa, …hebu jiulize kama wangekuwa na mawazo kama yako wangelifanya hivyo, ina maana wao kweli hawana uchungu na mtoto wao…?’ akauliza Maneno na kumwangalia Maua ambaye alikuwa bado anabubujikwa machozi kama mvua...

 Maneno akamtizama Maua kusubiri kuwa atasema lolote, alichoona ni mtu kamkodolea macho huku akiwa anatokwa na machozi, akasita kidgo kuongea lakini baadaye akasema `Maua leo niomekuja kwako maalumu kukuambia jambo muhimu sana, ….naomba unielewe, kuwa silisemi himi kwasababu ya shinikizo la matatizo yako, nalifanya kwa kuwa nina nia  nalo….’ Akasita kuongea na kumtizama Maua, cha ajabu alimuona akiwa bado kamkodolea macho, nay eye akatizama pembeni na kusema.

Maua hata kama unajiona kuwa umepona, lakini kwangu mimi, hata kwa shangazi yako na hata docta tumeliona hili kuwa bado hujapona, na docta kashauri kuwa bado una matatizo , matatizo ambayo yanahitaji mtu wa kuwa karibu naye wakati wote…lazimia uwe na mtu anayekufahamu fika, kwa mfano anaweza akaa rafiki yako akakuuliza mambo yaliyopita, akakurudishia uchungu, kaondoka wewe huku nyuma, ukaanza kubadilika na labda ni usiku, ukatoka na kwenda kusikojulikana…nakutolea huu mfano kwasababu huishi peke yako katika  hii dunia, watu kama hawo wasiokujua watatokea na kukuumiza moyo wako, licha ya kuwa nia yako ni kusahau kabisa, lakini ukikumbushwa hayo utakuwa unarejeshwa kwenye majonzi, na inawezekana kabisa yakatokea kama yale ya Arusha, na je kwa muda huo utakuwa na nani anayekujua vyema….. ‘ Maneno  akawa anaongea na kurudia rudia maneno kwa msisitizo, na akawa sasa kama anamsogelea, akijaribu kuona Maua atafanya nini akimsogelea karibu, lakini alichoona ni mtu kumtizama tu huku analia

Baadaye Maua akatulia na kupikicha macho yake, akawa kama vile kazindukana toka katika dimbwi lile la mawazo, akahema kwa nguvu, halafu akatizam tena kwa mbele, sasa akawa hamuoni yule aliyekuwa akimtizama mwanzoni, yupo Maneno , yupi sheei yake, ambaye analeta habari asizozitaka…..Maua alimtizama Maneno kwa mcho ya chuki, akawa kama anataka kumwambia usinisogelee, shetani mkubwa wee, lakini hayo yalikuwa akilini mwake, akawa anamwangalia tu kwa macho hayo ya chuki, yakiwa yamegubikwa na wingu la machozi…

‘Maua kwa ujumla kwa usalama wako unahitaji mtu wa kukaa nawe karibu, si usiku wala mchana, hebu nikuulize kweli ilikuwaje hadi ukatoka usiku kama ule hadi maporini sehemu ambayo usingeweza kwenda mwenyewe ukiwa na akili zako kamili, huoni kuwa umekumbwa na ule ugonjwa…ugonjwa unaomfanya mtu afanye matendo akiwa usingizini…, wewe ninavyokujua unaogopa sana nyoka hata kuitizama kwenye runinga hutaki, lakini siku ile ulikuwa nalo mwilini mwako, limekuzingira…hebu fikiria…kwa ujumla unahitaji mtu wa kuwa naye karibu, la sivyo tutasikia mengine, na mimi sitakubali hilo…’ akasema Maneno na moyoni Maua akasema ndio maana ukafanya ushetani wako huo, lakini hakutoa kauli hiyo kwa nguvu, hakutamani kuongea kwani kama angeliongea angesema maneno machafu na mwisho angekumbwa na balaa jingine, akabakia kimiya na hata kufunga macho yake.

‘Maua samahani najaribu kukurudisha nyuma, ili uone hatari iliyopo mbele yako…hebu jiulize wewe mwenyewe siku ile ulitokaje ndani na kutokomea maporini, na huku ushindwe kutoka na kutokomea mjini au hata baharini, na kwa ujumla hali kama hiyo unaweza ukawa uantembea bila kujali mgari au nini, kwasababu wazo lako linakuwa kufanya jambo moja, na mengine huyaoni…’ akasema Maneno…na hapo Maua akayafungua macho yake na kitu kama uwoga ukamwingia, kuonyesha naye anaikumbuka ile siku, ….analiona lile joka aliloliona kwenye njozi…ooh, sio njozi eti ilikuwa ni kweli…akazidi kufunua macho kwa woga, kama vile analihisi lile joka lipo karibu yake…

‘Sasa Maua nakuomba sana, sio kwamba nachukulia nafasi hii kama kisingizio, lakini …nafanya hili nikiwa nahitaji, nikiwa natamani, nikuwa na upendo wa dhati kwako. Mimi na Mhuja tulikuwa marafiki, tulikuwa tukipendana zaidi ya ndugu na wakati mwingine tulikuwa tukitaniana kuwa `mke wake ni wangu na mke wangu ni wake’ ulikuwa ni utani, lakini sasa naona imefikia mahali kukiri kuwa natamani iwe hivyo…naomba iwe hivyo…Maua nakuomba kwa mikono miwili nakuomba unipe nafasi ya Mhuja…’ akatulia na kumwangalia Maua.

Maneno alimshngaa Maua kuwa haonyeshi dalili yoyote ya kukubali au kukataa, na inaoenakan kama vile hayupo hapo kabisa, alikuwa katulia kimiya kama vile hajamsikia na Maneno akaendelea kuongea kwa kusema, `Mhuja kaondoka,na kiukweli kunahitajika mtu kuziba nafasi yake…na mtu huyo ni mtu anayekujali, anayekufahamu na anayekupenda kwa moyo wake wote, kama alivyokuwepo Mhua nap engine akakupenda zaidi yake, huwezi jua, …na Maua mtu huyo, hayupo mbali nawe, mimi ninakuahidi kuwa hutajijutia…nakuomba tafadhali unikubalie ombi langu la mimi kuichukua nafasi ya rafiki yangu mpendwa, …’ akasema Maneno a kushika kifuani kwake kwa mikono miwili.

‘Maua kiukweli mtu huyo anahitajika kwako haraka iwezekanavyo, na mimi ndiye ninayefaa, kwa sifa zote nilizozitaja, …hata hivyo baada ya tukio lile la Arusha, nimekuwa nikiteseka sana, kwasababu tendo lile lilitokea bila dhamira yangu…sikujiela ilikuwaje …na siwezi kuvumilia zidi na hata hivyo nitashindwa  kabisa kukuangalia machoni, najisikia uchungu sana, nasononeka sana….Nakuomba unisamehe kwasababu lile limetokea na huenda limetokea ili iwe hivyo..…’ akasema Maneno huku akimsogelea Maua na kuja kumpigia magoti...’

Maua alibakia akiwa kama kashikwa na mshangao, halafu akawa anawaza kwa undani nini alichoambiwa, na mara ile taswira ya Mhuja ikatokea tena mbele yake. Sasa hivi ila taswira ilikuwa kama anamwangalia kwa macho ya kutaka kujua atatoa kauli gani, na uso wa hiyo taswira ulionyesha chuki, ukiwa kama unasema `wewe ni msaliti, wewe umefanya nini, …’ Maua kuhis hivyo akageuza kichwa kutizama pembeni lakini akakutana na taswira ile ile, sasa ikimwambia `unaona ulivyo mnafiki, hata kuniangalia unaishindwa, kwasababu umenisaliti…wewe ni msaliti..’ akageuka huku na tena akakutana na uso kama ule ukimwambia; `haya toa jibu..toa jibu, …na jibu gani utaweza kulitoa wakati umeshafanya kwa vitendo, ..iliyobaki ni kauli kwa watu lakini kwa mtendo umeshatoa jibu…mkubalie msaliti mwenzako…kwaheri, nakutakia mafanikio mema…’ Maua liposikia maneno hayo kihisia akaanza kulia na kusema kwa sauti.

‘Hapana mimi sio msaliti  Mhuja, katu sikutarajia kufanya hivyo… na wala sikujua kuwa imekuwa hivyo…nilijua ni ndoto…hapana siwezi kukusaliti Mhuja, ….nakupenda mume wangu, nakuomba usiniache…nakuomba tafadhali,…sijui kilitokea kitu gani mpaka ikatokea hivyo…..sijui, na sijui na kitu gani kinanilazimisha kufanya hivyo….nakuomba Mhuja unisamehe, nipo tayari kuja huko ulipo, nipo tayari..hata sasa, nipo tayari…oooh, mungu wangu nimefanya nini…nisamehe mungu wangu….mungu wangu nakuomba unichukue roho yangu ikaonane na mume wangu…ooooh’ Akashikwa na kitu kama kizungu zungu akadondoka chini  na kupoteza fahamu...

Friday, April 1, 2011

Nani kama mama-26

‘Mwanangu safari yangu ya kwenda kutibiwa India ilinijia kwenye ndoto,  siku ile nilipokuwa nimezirai sijitambui, na kila hatua ilijionyesha wazi ndani ya ndoto, na kama ningekuwa najua kuwa ni kweli ningeliwaambia kuwa msiwe na wasiwasi, lakini sikuwa na uhakika nini tafsiri ya ile ndoto, kwani nilikuwa nusu mfu. Niligundua ukweli wa ile ndoto nilipokuwa nasubiri urekebishwaji wa sura yangu.
Nawashukuru sana wafadhili waliojitolea kuhakikisha narudia hali yangu ya awali, kwani sikuamini pale nilipoambiwa nijitizame kwenye kiyoo, ilikuwa kama najiona wakati nipo msichana…’ aliongea mama huku namtizama bila kuamini kuwa yule mama aliyekuwa na sura ambayo wengi waliamua hata kumuita mwanga kwa ajili ya michirizi na kuchanikachanika usoni, na sura kuwa ya kutisha, leo hii ni mwanamama mwenye sura ya kipekee…Mama mrembo na hayo macho…akajikuta akitabasamu akisema moyoni, ama kweli mama alijaliwa uzuri
‘Mungu ni mkubwa mama, siamini hadi sasa naona kama namtizama ndugu  yako, kwani sikumbuki kuiona sura yako ukiwa katika hali nzuri kama hii, mpaka uliponionyesha picha zako kabla ya kufanyiwa upasuaji na baada…kweli tuwashukuru sana wataalamu, tuwashukuru sana madakitari ambao fani yao  kwakweli ni ya kujali uhai wa mwanadamu…’ nikasema huku machozi yananilenga lenga
Mama akaongezea kusema, `Kumbuka nilikimbiwa, niliitwa mchawi, nikadharauliwa sababu ya  sura ile, ambayo sikupenda kabisa iwe vile, ila ni kwasababu ya watu wenye roho mbaya, na sijui baba yako huyo yupo hai au walimuua, maana kijijini kule kuuana ni kama jadi, na sijui yuke mwanamke wake atakuwa wapi, siku nikikutana naye …kutachimbika…’ mama akasema huku machozi yanamtoka, nami nikainua mkono na kumfuta yale machozi.
‘Mwanangu ndani ya ndoto yangu niliota kuwa upo katika hali mbaya, na  yale yaliyomfanya mama yako akimbiwe kuwa ni mchawi, yamekuandama kwa namna nyingine, watu wamekuwa wakikumbia eti  kwa vile wamekuona umekonda, wanahisi umeathirika….yote hayo  niliyaona kwenye ndoto kwa namna ya fumbo, lakini usijali mwanangu kwani yote hayo ni mitihani ya kimaisha, ikija unatakiwa uwe na subira, na usimamie katika haki…’ mama akanishika kichwa.
‘Mama unakumbuka uliwahi kunihadithia maisha yako ulipopitia na  nakumbuka ulikatisha siku ile ulipozidiwa ukashindwa kunimalizia kuwa ilikuwaje , je yule mama kule hospitalini alikuwa wewe  au nani na siku ile alipoondoka kule nyumbani kwa dada yake nesi alikwenda wapi na je alimpataje mtoto wake, na huyo mtoto ndio mimi au alikuwa mwingine…?’ nikamuuliza mawali mengi kwa pamoja.
Mama alimwangalia mwanae kwa muda, halafu akatabasamu na kusema, ‘hivi mwanangu bado una hamu na vidonda vinavyoonza kupona, huoni ukiyawaza hayo , ukayahadithia , yanatia simanzi , na mwishowe unakaribisha hasira za visasi, mimi naona  tusahau hayo tuganage yajayo…’Mama akasema akiinuka kuondoka
‘Mama ni vyema nikajua wapi nilipotokeaa ili niweze kujilinda, kwani nitasema mimi nilitokea wapi na kwa mafano baba akija leo kundai kuwa ni mwane nitamwambiaje…au…mama naomba unimalizie kile kisa kama hutojali..’ nikamsisitizia mama. Na mama akaniangalia tena , halafu akaanza kunihadithia pale tulipoishia.
‘Mwanangu, siku ile nesi na dada yake walijikuta wakifurahia ujauzito  ambao kwao ulikwa kama mgumba kupata mtoto, kiasi kwamba walijisahau nini kilichokuwa kimewaleta pale, na docta bosi wake alipoona vile akapendekeza nesi abakie pale siku ile hadi Jumatatu, kwani ilikuwa siku ya Ijumaa, na wao warudi mjini kama wataonana na yule mwanamke watamshauri afanye subira ili taratibu zifanyike za vipimo na mambo mengine, na kama mtoto ni wake atakabadhiwa. Wakakubaliana hivyo…na wao wakaondoka huku nyuma wakamuacha nesi akifurahia na ndugu zake.
Docta wao wakarudi mjini hospitalini, na walipofika hospitali wakakuta taarifa kuwa yule mama alifika, lakini safari hii alikuwa mpole na mstaarabu sana, akauliza mtoto wake yupo wapi, alipoaambiwa kuwa nyie mumeondoka kuja huko kijijini, akainuka kwa hasira na kusema,
‘Hivi mnafikiri kama ingekuwa nyie, mngefurahia hili mnalonifanyia, hivi kweli mnapenda mama atengane na mtoto wake hivihivi…sikubali, nitampata mtoto wangu mpende msipende…subirini…’ akaondoka, na haijulikani kuwa alielekea wapi.
 Docta na wenzake  walidhania kuwa huenda karudi huko kijijini na kwa vile walishaweka mambo sawa, haitakuwa na maneno, akifika huko ataelekezwa la kufanya. Siku ya Jumamosi kukawa na mawasiliano kati ya docta bosi wa nesi kumuulizia nini kinaendelea huko kijijini na kujua kama huyo mwanamke keshafika huko au bado! Cha kushangaza taarifa zilizofika ni kuwa yule mama hajaonekana huko kijijini, na wao walijua labda amekubali kusibiri huko hospitali …! Taarifa hiyo ikawaacha mdomo wazi na  kuwaacha kwenye mashaka kuwa huyo mama kaenda wapi!
‘Au kagundua kuwa sio yeye na mtoto sio wa kwake, na kaamua kuishia!..mimi bado nina mashaka nay eye…?’ akasema nesi
‘Lakini dalili na vielelezo vyote kama alivyotupa docta kijana vinaendana na yeye, sasa sidhani kama hoja ikawa sawa, labda…kama yupo mama mwingine mwenye sura kama hiyo…labda, …mimi naona tungoje, kama ndio yeye lazima atarudi tu, kama sio yeye basi tutakuwa na kazi ya ziada, ya kumtafuta mama halali wa mtoto, vinginevyo, inabidi uwaombe ndugu zako waendelee kumkubali huyo mtoto kama mtoto wao..’ akasema docta bosi wa nesi.
‘Hilo la ndugu zangu kumchukua huyu mtoto kama wao, sidhani kama litawezekana kwasababu shemeji yangu anasema akimwangali huyo mtoto anamkumbuka mbaya wake, kasababau wanafanana sana..’ akasema nesi.
‘Sasa ina maana shemeji yako anamjua baba wa mtoto, hawezi kuwasiliana naye..?’akauliza docta
‘Una maana chui awasiliane na mbuzi …inawezekana kweli…’ akaseme nesi kwa utani na wote wakaishia  kucheka. Na moyoni mwa nesi akawa anavutika na hisia zake za kumkumbuka docta kijana, na pia akimuwaza huyo docta kama angelikuwa mume wake ingekuwa ni furaha sana, …lakini docta huyo ni mume wa mtu…akajisemea moyoni kuwa docta kijana ndiye mume mtarajiwa…sijui kwa vipi!
Mazungumzo ya docta na nesi kwenye simu yaliishia bila kupata ufumbuzi wa maana, iliyobakia ni kusubiri tu nini kitatokea , kama huyo mama atatokea tena au kuna mama mwingine atakuja kujitambulisha yote kwao itakuwa heri, lakini lazima utaratibu ufuatwe ili, isije ikaleta mgongano baadaye…! Siku ya Jumamosi ikapita, na siku ya Jumapili ikaingia.
Ilikuwa siku ambayo wanafamilia walipnga kukutana  na siku hiyo waliipangia kuwa siku muhimu sana, waliamua kufanya kitafrija kidogo ambacho walikuwa mekipanga awali wakawa wanakiahirisha kwasababu hizi na zile, na hata walifikia kuwa wafanye tafrija hiyo baada ya kujifungua, lakini wakaona siku hiyo ya Jumapili inafaa, kifanyike tu. Waliona pamoja na hilo ni vyema, familia kama familia kukutana na kubadilishana mawazo, wakaitana wanafamilia wote waliopo karibu, na bahati nzuri , wanafamilia wengi walikuja , na ikaandaliwa tafrija fupi ya kumshukuru mungu kwa mama aliyekuwa hakutarajiwa kupata mtoto , sasa ni mja mzito, na mambo mengine ya kifamilia, na nesi akajiliza kichwani, hapo ni mimba tu, jei siku akizaliwa huyo mtoto itakuwaje…
Pilika pilika zikaanza, watu na majirani wakajumuika na wahusika wakaitambulisha ile tafrija fupi kuwa ina maana gani.
Wakati watu wamejimwaga na vyakula vinaliwa, hakuna aliyekuwa na wazo lolote zaidi ya ile sherehe, dada wa nesi na nesi walikuwa wamevalia sare, na mume mtu alikuwa kavalia suri yake safi wakawa wamekaa pale mbele kama wahusika wakuu, picha za kumbukumbu zikapigwa.
‘Mwiteni mtoto wetu  naye apate picha ya kumbukumbu…’ akasema dada wa nesi, akiwa na mama yule mtoto wa kufikia na hata nesi akasema hivyo. Hoja hii aliipinga shemeji mtu, akaondoka pale walipokuwa wamekaa na kuitenga,  kwani tangu mtoto yule achwe hapo, amekuwa hana raha kabisa. Na alikuwa mbalimbali na huyo mtoto, na ikitokea bahati wakakutana , yeye humkwepa, licha ya kuwa mtoto kila mara alikuwa akimlilia na kumuita `baba, baba…’
Kuna mara nyingine aliingiwa na huruma na kumchukua , na akimtizama usoni ,…anakuwa kama anakumbuka kitu, basi humwachia …na hutafuta mwanya wa kutoka hapo nyumbani , na kwenda zake nje kukutana na marafiki zake. Mkewe alimshauri sana kuwa anachofanya siyo jambo la kiungwana, kwani yule mtoto hana kosa kabisa, ni kimumbe ambaye hajui kabisa nini kilitokea…mumewe anamjibu kuwa yeye hajui machungu gani aliyoyapitia , na mtoto huyo humtonesha donda ambalo lilishaanza kupona! Na mazungumzo hayo hayaishii vyema, mume mtu anaamua kuodnoka, ili wasiendelee kubishana
‘Mtoto haonekani…’ akasema dada mmoja ambaye ni ndugu kwa kupitia kwa babu  yao,  yaani baba yake nesi na baba wa huyo dada wanazaliwa tumbo moja kwahiyo kiutaratibi huyo dada anamwita nesi au dada yake nesi `dada ’ wao wanaishi kijijini ambapo familia yao ndipo ilipoanzia na alikuja hapo toka huko kijiji kingine kwa ajili ya kuishi na ndugu zao hawo kwa vile dada yao ni mja mzito basi aliletwa kuja kusaidia kazi mbalimbali.
‘Umemwangalia huko alikokuwa akicheza na wenzake..’ akauliza nesi
‘Kote nimeangalia na nimewauliza wenzake wanasema hawajui wapi ameenda, wengine wanasema aliondoka kuwa anakuja ndani kunywa maji lakini hakurudi tena,, wengine wanasema alikuwa akiangalia ngomea iliyokuwa ikipita , na huenda ameongozana nayo…’ ilimradi kila mtoto alisema lake. Ikawa shughuli kumtafuta mtoto kaenda wapi. Mpaka inafika usiku haijulikani wapi mtoto kaelekea.
‘Sasa tutafanyaje maana hii sasa ni kesi akija mama wa mtoto tutamwambia nini…’ akaanza kulalamika nesi
‘Bwanae, naona unataka kutuharibia tafrija yetu, niliwaambia huyo sio daamu yetu atatuletea mabalaa hamtaki kusikia, anagalieni tangu aletewe hapa, kila mara linazuka jambo la utata..mnaona sasa, …mimi simo kwa hili na wala msinishirikishe, maana huyo mwanamke balaa akija hapa atanizukia mimi na kuniletea mambo nisiyo yataka…’ akasema shemeji mtu.
‘Hili ni letu sote kwasababu mtoto huyu aliachwa hapa kwenye nyumba yako, huwezi kulikwepa cha muhimu ni kusaidiana jinsi ya kumtafuta , na bora tuwape taarifa polisi…’ akasema mke mtu.
‘Nani aende polisi, yaani nipoteze muda wangu kwa ajili ya….’ Aksema mume mtu na kabla hajamaliza simu ikaiita, na nesi alipoitizama simu yake akakuta anayeiita ni docta, akasogea pembeni huku akiwa na wasiwasi atamwambiaje huyo docta bosi wake ambaye alishachukua dhamana ya usalama wa huyo mtoto!

Jamani sio kwamba napenda kuandika kiduchu, bali ni majukumu, na sipendi siku ipite bila kuwakilisha angalau kidogo, na hi ni sehemu amabayo ilibakia nyuma, kwani mhadithiaji  alikuwa mama wa jamaa anayetupa hiki kisa na huyu mama alikuwa kapekwa India, …tuendelee kuwepo ili tukamilishe hiki kisa na kama kuna sehemu nimeruka naomba mnihabarishe, ili tumalizie vyema! Karibu sana, na kumbukeni maoni yenu ndiyo yatakayofanya kisa hiki kiwe na mwisho wenye mvuto zaidi!

Monday, May 24, 2010

Je huu ndio wajibu wa ndoa!

`Mimi najuta kuolewa, nashangaa nyie mnaolalamika kuwa hampati waume wa kuwaoa, mngelijua kasheshe, suluba, bugudha na utumwa uliopo humo ndani mwa kitu ndoa, mngelifikiria sana hili swala la ndoa, na ni bora ukawa na uhakika na huyo unayemtaka. Lakini hata hivyo, mbona mimi nilikuwa na uhakika huo, lakini siku nilipotumbukiza mguu wangu ndani ya nyumba ya ndoa, nilitamani mlango ufunguke nitoke nje, lakini ilikuwa nimeshachelewa…’ Hii ilikuwa hotuba ya mama mmoja kwa wenzake waliokuja kumtembelea.

`Hapana, usemayo unaangalia upande wako tu, hebu tueleze ni masibu gani yaliyokukuta, ili nasi tujihami nayo?’

‘Siku nilipofika nyumbani kwa mume wangu, nilikaribishwa na mawifi na shemeji zangu kwa sangwe, kwenye jumba kama la kathiri, humo wanaishi familia yote. Mwezi ule wa kwanza, nilijiona kama malkia ndani ya nyumba ya mfalme. Kila kitu kilikuwepo, lakini wao hawakutaka kuweka mfanyakazi wa nyumbani, waliniambia kuwa kwasababu wao wapo hakuna haja ya kumuajiri mtu, nikakubaliana nao, kwani hata nilipotoka hatukuwahi kuajiri mfanyakazi wa ndani, huwa tunajituma wenyewe!

Mara mume akaondoka ki-kazi, yeye hufanya kazi za masafwa marefu, kwahiyo akiondoka, hukata mwezi, akirudi hukaa siku mbili au tatu, na huondoka tena. Alipoondoka, nilishangaa, watu wote wakawa wananituma mimi kazi, mara wifi tuna njaa, mara shemeji leo utatupikia nini, waume zako tuna njaa. Mimi kwasababu nimezoea kazi, nikawa nafanya watakavyo.

‘Kila akiondoka, mimi hugeuka mtumwa, nafanya kazi zote za ndani, kuhudumia familia, kuwalisha shemeji zangu na mawifi, wao hulala, hujikalia au kutembea. Cha ajabu ndugu yao akirudi wanakuwa tofauti, hufanya kazi zote na mimi hawaniruhusu kugusa kitu, na kumwambia ndugu yao kuwa wao hawataki kumtesa wifi au shemeji yao. Hiki ndichi kilichoniuma, kwanini hawasemi ukweli, nisingechoka mapema hivyo, ila unafiki wao ndio ulioniuma sana….’

‘Niliamua kumweleza ndugu yao kinamna, nikiogopa kuigombanisha familia, na ndugu yao ambaye ni mume wangu alishangaa na kusema, mbona nikiwepo sijaona wakikuruhusu kufanya kazi, mbona nashindwa kuelewa kwasababu wao wenyewe wananiambia, wewe hawakuruhusu kabisa kufanya kazi, wanakuhudumia, kukufulia , kukupikia nk…’ kaka mtu hakuamini.

`Kama huamini basi, ila ukweli ndio huo ninaokueleza, ndugu zako ni wanafiki, hugeuka kama kinyonga. Nisingekueleza haya kama wangesema ukweli, lakini yote ni heri ipo siku utajionea mwenyewe’ nikajitetea.

‘Siku anaondoka kesho aliwaita kikao nakuwasema, na wao walijitia kushangaa, na kusema hilo halipo na halitatokea. Akaondoka, baadaye wanafamilia waliniita bila kaka yao kuwepo na kuniuliza, kuwa kuna tatizo gani, kwani wao wamefanya kipii kigeni, wakasema, kaka yao akiwepo inabidi wafanye kila kitu ili wanipe muda wa kukaa mimi na mume wangu, lakini akiondoka, inabidi na mimi nisaidie kazi za nyumbani…wakasema, kama naona kazi ni nyingi , nifanye ninazoweza. Wakaongezea, wao wanafikiri kufanya hivyo ndio wajibu wake, ndio wajibu wako katika ndoa. Wakamalizia kwa kuniomba samahani, halafu wakatawanyika na tabia ikawa ile ile!

‘Huo ndio wajibu wa ndoa nyie mnaotaka kuolewa’ akamalizia Yule mama.

Haya ni baadhi ya madhila katika ndoa, na wengi wakiyapata hukimbilia kuilaumu ndoa, lakini tujiulize kiuweli haya ndio masharti ya ndoa, na je yakitokea ndio sababu ya kuihujumu ndoa kuwa haifai? Hapana, hayo ni mawazo ya ubinafsi na tusiyachukulie kama msingi wa ndoa. Ndoa ni sehemu inayokamilsha ubinadamu, kuwa mwili mmoja, na kila mmoja ajihisi nafasi sawa na mwingine. Jamabo la muhimu ni kushirikiana, kuambizana na kuvumiliana.

Na kwa hili lilomkuta huyu mama nafikiri ni vyema angemmshauri kaka yake afanya uchunguzi na pindi akigundua kama kweli ana hekima na upendo atalisuluhisha na huo wajibu wa ndoa utawekwa sawasawa. Kuna haja ya kuelezana hili kiundani siku tukipata nafasi.